1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa Kisudan 1,000 watoroka kambini Ethiopia

Sudi Mnette
4 Mei 2024

Takriban wakimbizi wa Kisudan 1,000 wamekimbia kambi inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa kaskazini Ethiopia kufuatia mfululizo wa matukio ya ufyatuaji risasi na uporaji.

https://p.dw.com/p/4fUv6
Ethiopia Tigray Shire | Kambi ya wakimbizi ya Eritrea
Kambi ya wakimbizi ya Shire nchini EthiopiaPicha: Joerg Boethling/IMAGO

Inaelezwa watu 7,000 kati ya wakazi 8,000 wa eneo hilo la Kambi ya Kumer walianza safari kwa miguu tangu Jumatano baada ya kushambuliwa na kufanyiwa uporaji na wanamgambo wa eneo hilo.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao wamesema walizuiliwa na polisi muda mfupi baada ya kuondoka kambini eneo la umbali wa kilomita 70 kutoka katika mpaka wa Sudan katika eneo la Amhara nchini Ethiopia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema linafahamu kwamba watu 1,000 walikuwa wameondoka katika kambi ya Kumer Jumatano iliyopita kwa sababu walihisi kutokuwa salama baada ya mfululizo wa matukio ya mashambulizi.